loader
Kilimanjaro yavuna mabilioni ya fedha

Kilimanjaro yavuna mabilioni ya fedha

FEDHA za Maendeleo zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu kwa Mkoa wa Kilimanjaro katika kipindi cha miezi sita zimevunja rekodi.

Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha la utamaduni kwenye uwanja wa Ushirika, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema  katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2021, mkoa huo umepokea Sh bilioni 57.39  sawa na asilimia 40 ya bajeti yote ya maendeleo.

“Hiki ni kiwango kikubwa cha fedha za maendeleo kuwahi kupokelewa mkoani hapa katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa Serikali. Kwa niaba ya wananchi wa Kilimanjaro tunakushukuru sana, mh Rais”amesema.

Amesema awali mkoa huo ulipokea Sh bilioni 7.88 ambazo ni sehemu ya mkopo wa Sh trilioini 1.3  kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa ajili ya ustawi na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Pia mkoa huo umepokea ia mkoa huo umepokea Sh bilioni 2.48 zinazotokana na tozo kwenye miamala ya simu, Sh bilioni 18 za ruzuku ya maendeleo kwa Serikali za mitaa na pia mkoa ulipata Sh billion 4.2 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za Kata.

Hali kadhalika mkoa huo ulipokea Sh milioni 418.1  ambazo ni fedha za mpango wa matokeo, Sh bilioni 22.44  kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara na ukapokea Sh bilioni 1.9 kwa ajili ya miundombinu ya maji katika mkoa huo.

Aidha, Kagaigai amesema fedha zote zilizopokelewa zimeelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya utoaji wa huduma  katika sekta za Afya, Elimu, Maji, barabara na madaraja.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d5b2857535bd794dac7eb6c3f8c12bca.png

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi