loader
Mabeyo azindua kituo cha mafuta, ataka jeshi kuwa wabunifu

Mabeyo azindua kituo cha mafuta, ataka jeshi kuwa wabunifu

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo amewataka viongozi wa jeshi hio kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii na uadilifu.

Jenerali Mabeyo ameyasema hayo wakati akizindua kituo cha mafuta kilichojengwa na Kikosi cha R971 cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo Dodoma ambapo nimmoja wa mradi wa kikosi hicho wa kujiongezea kipato.

“Tunaweza kufanya mambo makubwa sana. Kinachotakiwa ni kujiamini kwamba tunaweza na kubadili mitazamo yetu iwe chanya wakati wote. Tunatakiwa kuwa wabunifu lakini pia kuwa waadilifu katika hii miradi” Amesema.

Jenerali Mabeyo pia amewataka makanda wa vikosi mbalimbali vya jeshi kuhakikisha wanatumia vyema taaluma na vipawa walivyo navyo askari wa jeshi hilo ili kuwa na miradi yenye ubunifu ambayo itapunguza utegemezi wa jeshi hilo kwa serikali.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c18578dfda77e0281c88c50bd48131b7.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi