loader
Hapi: Toeni vibali maeneo yote ya miradi

Hapi: Toeni vibali maeneo yote ya miradi

HALMASHAURI za Mkoa wa Mara zimeagizwa kuzipatia hati miliki maeneo yote yanayojengwa miradi ya vituo vya afya na shule ili kuepusha migogoro ya mipaka.

Mkuu wa Mkoa huo, Ali Hapi ameagiza hayo leo  baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya Bumera, katika Halmashauri ya Tarime.

RC Hapi pia ameagiza mamlaka zinazotoa huduma za barabara, maji na umeme kuanza kupeleka huduma hizo kwenye maeneo hayo ili ujenzi ukikamilika wananchi waanze kuhudumiwa.

Awamu ya kwanza ya ujenzi wa Kituo hicho unatarajiwa kukamilishwa Machi 14 Mwaka huu kwa Sh milioni 250 zilizotokana na tozo za miamala ya simu, inayofanywa na kila mwananchi.

Msimamizi wa Mradi huo, Mangu Mahero amesema katika awamu hiyo wanajenga maabara kwa Sh milioni 80, jengo la wagonjwa wa nje kwa Sh milioni 160 na kichoma taka kwa Sh milioni 10.

Amesema awamu ya Pili itagharimu kiasi kama hicho cha fedha, ambazo kwa mujibu wa RC Hapi zitapokewa mwezi ujao (Februali) na itajenga majengo mengine matatu likiwemo Jengo la Upasuaji.

Amesema huduma za upasuaji zitapunguzia wakina mama usumbufu, ambao wamekuwa wakipewa rufaa kwa wastani wa zaidi ya 800 kwa mwaka, wengi wakihitaji huduma za uzazi.

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Tarime, Daudi Ngicho amesema pamoja na wananchi wa Kata hiyo,  kituo hicho kitahudumia wakazi wa kata jirani zikiwemo Kata za Utegi ya wilayani Rorya, Nyandoto ya mjini Tarime na Susuni.

Ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwamba imewaheshimisha, kwa kutekeleza ahadi walizotoa kwa wananchi, wakati wa uchaguzi mkuu uliyopita, kwamba saaa wanatembea kifua mbele.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9ed73c7f3644f437b2128f3feafdaf89.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi