RAIS wa Serikali ya Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Kitaifa yatakayofanyika leo kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Akizungumza na vyombo vya habari juzi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka alisema uzinduzi utafanyika leo. Maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika Januari 23 hadi 29 mwaka huu.
Sherehe za uzinduzi huo zitaanza kwa matembezi yatakayoanza saa 12:00 asubuhi kwenye viwanja vya kituo jumuishi cha haki na kuishia kwenye viwanja vya Nyerere Square ambapo sherehe za uzinduzi zitafanyika.