loader
Serikali kukomesha ukatili kijinsia kwa wanafunzi

Serikali kukomesha ukatili kijinsia kwa wanafunzi

SERIKALI imeandaa mpango mkakati wa kuanzisha dawati la kijinsia kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyogharimu maisha ya wanafunzi.

Aidha,  imesema wanafunzi wa vyuo vikuu na kati wamekuwa waathirika wakubwa wa vitendo hivyo vinavyosababisha uzorotaji wa masomo yao.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Doroth Gwajima alisema hayo wakati akizindua  dawati la kijinsia na mradi wa Our Right, Our Lives, na Our Future (03) unaofadhiliwa na Shirika Umoja Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco ).

Alisema  serikali itahakikisha kuanzia vijijini kunakuwa na mifumo madhubuti ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.

“Kuna matukio mengi ya ukatili wa kijinsia  yanaongezeka hivyo wakati umefika sasa wa kutokomeza haya yote kwa kuwepo kwa dawati la kinjinsia kila chuo,” alisema na kuongeza kuwa madawati hayo yanatakiwa kuwa madhubuti na yanayofanya kazi kwa vitendo.

Hata hivyo alisema serikali haijawahi kukaa kimya kuhusu ukatili unaoendelea katika vyuo na ilishaanzisha vituo mbalimbali vya kisheria.

Naibu Waziri wa Elimu,  Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga alisema mradi wa 03 utanufaisha v Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Makamu Mkuu wa UDSM , Profesa William Anangisye alisema mradi wa 03 una malengo matatu ambayo ni kuondoa ndoa za utotoni, kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutokomeza  ukatili wa kijinsia katika vyuo vikuu.

Mkurugenzi Mwakilishi wa Unesco nchini, Tirso Santos alisema lengo la kuleta mradi huo ni kutaka kuona wanafunzi wa vyuo vya juu wanasoma huku wakijiamini.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f23dcbc72e907436403a6aba89ebdc70.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi