loader
Simba yavutwa, Azam mambo safi

Simba yavutwa, Azam mambo safi

SIMBA imelazimishwa suluhu dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa ugenini kwenye Uwanja wa Manungu Turiani mkoani Morogoro jana.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 25 katika michezo 12, huku Mtibwa ikiendelea kusalia nafasi za chini ya 13 kwa pointi 12.

Wekundu hao watazidi kujiweka katika presha dhidi ya mpinzani wake Yanga anayeongoza kileleni kwa pointi 32 na ikiwa itashinda mchezo wa leo dhidi ya Polisi Tanzania itaachwa kwa tofauti ya pointi 10 ila Simba bado ina kiporo kimoja.

Simba ilimiliki mpira dakika zote 90 za kutengeneza nafasi kadhaa, lakini hawakuweza kuzitumia ipasavyo.

Pengine mazingira ya uwanja uliokuwa na maji umewanyima nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa wachezaji walionekana kushindwa kuendana na kasi na mpira kubaki nyuma na wengine wakiteleza.

Mtibwa walikuwa wanalinda goli muda mwingi sambamba na kucheza mipira mirefu isiyokuwa na faida wakionekana wazi kuwa walihitaji sare.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Chris Mugalu, Hassan Dilunga, Gadiel Michael, Mzamiru Yassin, Henoc Inonga  na kuingia Bernad Morrison, Cleatous Chama, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, John Bocco yalisaidia kuongeza mashambulizi lango ni kwa Mtibwa ila hayakuzaa matunda.

Mtibwa pia, iliwatoa Kelvin Sabato, Salum Kihimbwa na Said Ndemla na kuingia Baraka Majogoro, Nassoro Kiziwa na Joseph Mkele nayo hayakusaidia zaidi ya kuimarisha kwenye ulinzi.

Mchezo mwingine Azam FC iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa katika uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga.

Mabao ya Azam yalifungwa na Teps Evance, Charles Zulu, Ibrahim Ajibu na Ismail Kada.  Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kusogea taratibu nafasi za juu ikitoka ya tano hadi ya nne kwa pointi 21.

Timu ya Biashara United ililazimishwa suluhu dhidi ya Geita Gold katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara. Wenyeji bado wanaendelea kushika mkia.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/19dc222c147d0c5b5baae8de5a501239.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi