loader
Rais Samia akoshwa na wasanii

Rais Samia akoshwa na wasanii

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema anafarijika kuona wasanii wakishiriki katika vinyang’anyiro mbalimbali katika majukwaa ya kimataifa na baadhi yao kushinda tuzo.

Aidha, alisema anafarijika kuona nchi ikichangamka kwa matamasha mbalimbali na namna vijana wakiitwa kwenda kufanya majaribio katika nchi mbalimbali.

Rais Samia aliyasema hayo Moshi mkoani Kilimanjaro jana kwenye  Tamasha la Utamaduni mkoani humo.

“Katika sanaa na utamaduni, tunafarijika kuona wasanii wetu wakishiriki katika majukwaa ya kimataifa na baadhi yao hushinda na kuleta tuzo hapa nchini,”alisema.

Miongoni mwa wasanii waliowahi kushiriki matamasha mbalimbali ya muziki ya kimataifa ni Rajabu Abdul ‘Harmonize’ Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Faustina Charles ‘Nandy’ katika mataifa ya Dubai, Marekani, Ghana, na Ureno.

Pia, wasanii hao wamewahi kutwaa tuzo mbalimbali wakiongozwa na Diamond Platnumz aliyewahi kutwaa tuzo za msanii bora Afrika Mashariki za Afrimma, tuzo za MTV Mama na MTV Europe kwa vipindi tofauti.

Katika hatua nyingine, Rais Samia alihimiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea kuratibu, kuvikuza na kuviendeleza vikundi vya burudani vya kiutamaduni.

Pia, aliitaka Wizara hiyo ihamasishe mashindano ya tambo, tenzi, nahau, na ushairi, ukitumia mila na usanifu wa lugha ya Kiswahili.

Alisema Mei mwaka huu kutakuwa na tamasha la kitaifa la utamaduni litakalokusanya mikoa yote na kuagiza matayarisho yawe mazuri, yaandaliwe kimkakati ili kuwavutia wageni kutoka nje kuja kuona utamaduni wa hapa.

Alitolea mfano matamasha kama hayo yaliwahi kufanywa  Rio Samba Brazil kuwa ni tamasha linalovuta watu na Ujerumani pia,  huhudhuriwa na watu kati ya milioni tano hadi sita na lile la Sauti za Busara Zanzibar huleta pia wageni wengi huku akihimiza lile la Bagamoyo liwekwe vizuri na kutangazwa kuwavutia watu wengi wa kimataifa.

Rais Samia alisema wataendelea kuimarisha bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili iwe na uwezo wa kubaini, kulinda na kutangaza mila na desturi za nchi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a346b58d12b947922d16940640b2f25f.jpg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi