loader
Dk Yonazi ataka ufanisi, kasi mradi wa anuani

Dk Yonazi ataka ufanisi, kasi mradi wa anuani

KATIBU Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi amewataka wataalamu waliojengewa uwezo kuhusu anuani za makazi kutumia mafunzo hayo kwenda kutekeleza kwa ufanisi mradi huo ili kufi kia lengo la serikali la kukamilisha mfumo huo kabla ya Mei mwaka huu.

Dk Yonazi ametoa rai hiyo jana wakati wa kufunga semina ya siku saba ya kujenga uwezo watalaamu wa mikoa na halmashauri juu ya anuani za makazi yaliyofanyika Tanga, Mbeya, Mwanza na Zanzibar.

Alisema ni vyema wataalamu hao wakatumia utaalamu wao kutekeleza kwa vitendo utekelezaji wa mfumo huo ili kutimiza azima ya serikali ya kukamilisha mfumo huo ifikapo Mei mwaka huu.

“Jambo la anuani za makazi ni jambo la kitaifa lenye maelekezo na lina ukomo kwa utekelezaji na ninyi ni wataalamu mnaokwenda kuisaidia serikali kufikia azma ya kukamilisha utekelezaji wa mfumo kabla ya Mei, 2022,”alisema.

Dk Yonazi alitoa wito kwa viongozi na waratibu wa mradi huu katika ngazi ya wizara zinazotekeleza kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega na wataalamu hawa waliohitimu katika kutatua changamoto mbalimbali zitakazojitokeza wakati wote wa utekelezaji wa suala hilo.

Aidha, Dk Yonazi amewataka kuhakikisha wanasimamia kikamilifu mambo kadhaa yakiwemo ya kuhakikisha wanashirikisha vyema wakurugenzi na viongozi wengine kuhusu umuhimu na kasi ya utekelezaji inayohitajika ili kuwe na uelewa wa pamoja.

Pia kuhakikisha kuwa mipango kazi waliyoiandaa katika mafunzo wanashirikisha viongozi wao ili waimiliki mipangokazi na wasimamie utekelezaji wake kikamilifu.

Alisema pia wahakikishe wanakwenda kujenga uwezo kwa wataalamu wa ngazi zote ili nao washiriki katika kufanikisha suala hili na kuendelea kuhamasisha wananchi na wadau wa maendeleo kujiwekea miundombinu ya mfumo katika maeneo yao.

Pia aliagiza kuhakikisha taarifa ya utekelezaji zinafika ofisini kwake kila baada ya wiki mbili kutoka katika halmashauri kuanzia jana. Naye mratibu wa anuani za makazi na postikodi kitaifa, Jampyoni Mbugi alisema mafunzo hayo yametolewa kwa vitendo ikiwa ni utoaji wa anuani na kuingiza taarifa za makazi kwenye mfumo.

Alisema mafunzo hayo yameshirikisha wataalamu 419 kutoka halmashauri 163 na mikoa 12 ya Zanzibar.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1242b888a94bc8ddff911f54b33ae83f.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi