loader
Nyumba 36, shule 2 zaezuliwa paa

Nyumba 36, shule 2 zaezuliwa paa

NYUMBA 36 zikiwemo shule mbili za msingi za Makombe na Bwilingu katika Jimbo la Chalinze mkoani Pwani zimeathirika kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua mapaa hivi karibuni.

Akizungumza na waathirika wa tukio hilo katika Kijiji cha Makombe, Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete, mbali na kuwapa pole, pia alisema kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, wataangalia namna ya kuwasaidia waathirika ili warejee kwenye maisha yao ya kawaida.

“Binafsi nimesikitishwa na janga lililotokea lakini wakati mwingine tuamini kila jambo limepangwa na Mwenyezi Mungu na lina sababu zake. Namshukuru Mungu kwa sababu katika taarifa yenu hakuna mtu aliyeumia,” alisema.

Kutokana na uharibifu wa madarasa katika Shule ya Msingi Makombe, Ridhiwani aliagiza zifanyike jitihada za haraka za kuyarejesha madarasa hayo katika hali yake ya kawaida ili wanafunzi waendelee kuyatumia.

Pia alitoa Sh milioni tano ili kusaidia kurekebisha sehemu zilizopata athari ya mvua ili wanafunzi waendelee na masomo. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhani Possi, alimweleza Ridhiwani kuwa baada ya tukio hilo, ofisi yake ilichukua hatua mbalimbali ikiwemo kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea na kuahidi ndani ya wiki moja madarasa hayo yataanza kutumika.

“Katika kijiji cha Makombe tatizo ni kubwa zaidi na tumeanza kuchukua hatua na leo(jana) Mbunge ametuongezea nguvu, katika gharama ya shilingi milioni 26, ametuongezea shilingi milioni tano,”alisema Possi.

Diwani wa Bwilingu, Nasser Karama, alisema mvua hiyo pia imewaathari baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Bwilingu pamoja na Shule ya Msingi Bwilingu ‘A’.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7a3e7dcb77da111bb4c216792dced4eb.PNG

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Chalinze

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi