loader
Soko la bidhaa za kilimo  China fursa kwa Tanzania

Soko la bidhaa za kilimo China fursa kwa Tanzania

KATIKA ukurasa wake wa habari za kimataifa jana, gazeti hili liliandika kuwa: ‘China yafungua fursa ya soko la bidhaa za Afrika,’ huku bidhaa lengwa zikiwa za kilimo.

Katika habari hiyo, gazeti hili lilimnukuu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wu Peng akisema nchi hiyo imetangaza kufungua mpango maalumu wa soko la bidhaa za kilimo kutoka Afrika.

Wu alisema sekta ya kilimo inahitaji maendeleo makubwa kwa kuwa bila kilimo cha kisasa maendeleo ya viwanda hayawezekani.

Soko hili la bidhaa za kilimo nchini China ni fursa muhimu kwa Tanzania kutokana na uwezo wake wa kuzalisha kiasi kikubwa cha mazao mbalimbali ya kilimo lakini hasa mahindi.

Mara kadhaa Serikali imekuwa ikisema kuwa, kama nchi tuna kiasi cha kutosha cha chakula na ziada inayoweza kuuzwa nje ya nchi. Kwa kuwa kumekuwa na uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi hapa nchini, ni vyema wizara zinazohusika pamoja na Bodi ya Mazao Mchanganyiko zikafuatilia kwa karibu jambo hili ili wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania wanufaike na soko hilo la bidhaa za kilimo nchini China.

Katika hotuba yake ya mwezi Septemba mwaka jana ya kutoa taarifa ya serikali kwa wananchi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alisema kiasi cha mahindi kilichozalishwa kilifikia tani milioni saba wakati mahitaji ya ndani ni kati ya tani 570,000 hadi tani 580,000 kwa mwaka.

Tani milioni saba za mahindi ni kiasi kikubwa ikilinganishwa na mahitaji ya ndani kwa mwaka, hivyo kama Tanzania itafanikiwa kulikamata soko hilo la bidhaa za kilimo la China, itakuwa ukombozi mkubwa kwa wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye ardhi bora inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwamo ya nafaka, matunda, mboga na mengine mengi, hivyo ujio wa soko hilo la China ni fursa kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao hayo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/21af107d2a809f6851d7351c04846870.jpeg

MOJA ya misemo maarufu ya Rais mstaafu Ali Hassan ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi