loader
Taasisi ya Ustawi wa Jamii inavyowajengea uwezo mabinti wanafunzi

Taasisi ya Ustawi wa Jamii inavyowajengea uwezo mabinti wanafunzi

Chama cha wanafunzi wa Kike wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii-ISW (AWESOME YOUTH VISION GROUP) iliyopo Kijitonyama, Dar es Salaam ambayo iko chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kimefanya kongamano la mabinti kumjengea uwezi mtoto wa kike.

Kongamano hilo limefunguliwa na Mhadhiri Msaidizi Kutoka idara ya Ustawi wa Jamii Taaluma Bi. Rufina khumbe kwa niaba ya Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt.Joyce Nyoni.

Akifungua kongamano hilo Bi Rufina amesema thamani ya mwanamke ni kubwa duniani hivyo anapaswa kujitambua, kujithamini na kuachilia baraka ambazo Mungu amempatia kwa kufanya yaliyomema na kukubalika na jamii yake.

"Thamani ya mwanamke ni asili kupitia maandiko ambapo Mungu alibaini uhitaji wa mwanamke na ndipo akamtengeneza kukamilisha uumbaji. Kibali na baraka za mwanaume na jamii zipo kwa mwanamke hivyo binti ni dhahabu na lulu," amesema Bi Rufina.

Lengo kuu la kongamano hilo ni kumnyanyua binti; kwa kumpa elimu na kumjengea uwezo wa kujitambua na kuwa na ujasiri wa kuthubutu na kutumia fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na elimu, uongozi, kupaza sauti kwa niaba ya mabinti wenzake, kujiamini na kujisimamia pamoja na ujasirimali.

Sambamba na hilo pia wanafunzi wa kike wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii walipatiwa elimu kuhusiana na nidhamu na maisha kipindi ambacho wapo Taasisi hiyo na namna sahihi ya kuweka malengo, nidhamu na namna ya kukabiliana na changamoto za mazingira, na kuweza kufikia malengo.

Mada mbali mbali ziliwasilishwa na wachangia mada waalikwa ambapo "Elimu juu ya haki na usawa wa kijinsia" iliwasilishwa na mwalimu Sophia Mbeyela kutoka Shule ya Msingi Kijitonyama wakati Mkurugenzi wa Amani ProjectVile aliwasilisha mada kuhusu watu wenye uhitaji maalum.

Mada ya Elimu ya Afya na maadili iliwasilishwa na mwanzilishi wa Be Hamble project na mtangazaji wa redio, Asumpta Godfrey. Mada ya elimu juu ya binti kutambua fursa na kuzitumia hasa anapokuwa chuo na namna sahihi ya kujiwekea malengo na kuhakikisha kufikia malengo ilitolewa na Asma Jamida kutoka Wasafi media.

Kwa upande wake Shamira Mshangama kutoka Wasafi Tv alizungumzia uongozi na mwanamke namna ambavyo binti anaejitambua, kujithamini na kujiwekea malengo anaweza kuwa kiongozi bora kutoka ngazi ya Taasisi hadi Taifa nini afanye na kuepuka, mbinu na taratibu za kufanya; changamoto na namna ya kukabiliana nazo.

Taasisi ya Ustawi wa Jamii inatambua nafasi kubwa iliyonayo ya kutoa elimu bora ya kitaaluma kwa wanafunzi inayowaandaa kuhudumia jamii lakin pia kutoa elimu kwa jamii inayozunguka Taasisi na Jamii ya watanzania kwa ujumla ili kupunguza matatizo ya Kijamii ya mtu mmoja mmoja, familia, na makundi maalum kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan aliona upekee katika ustawi wa jamii na kuunda wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Taasisi ya Ustawi wa Jamii itaendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari, vyumba vya mihadhara ya kitaaluma na Kituo chake cha elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia pamoja na mikutano na wanajamii ili kupunguza vitendo viovu na vya ukatili kwa Watoto, wanawake na makundi maalum vinavyoendelea kushamiri hapa nchini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/70fee2c352e56980a4c44889f7eb5575.jpg

MATUMIZI mengi ya bidhaa za tumbaku ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi