loader
Vijana watano mbaroni  mauaji ya wanawake 3

Vijana watano mbaroni mauaji ya wanawake 3

J ESHI la Polisi mkoani Mwanza limewatia mbaroni vijana watano wanaotuhumiwa kuhusika kuua wanawake watatu wa familia moja kwa kutumia mapanga.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ramadhan Ng’azi alisema jana kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa baada ya polisi kufanya uchunguzi kwa siku tano kuanzia Januari 19 hadi 23, mwaka huu. Alisema watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika kuwaua wanawake hao wakazi wa Mecco, wilayani Ilemela Januari 18 mwaka huu, saa 5.30 usiku.

“Watu hao tumewakamata wakiwa na vielelezo mbalimbali zikiwamo mali za marehemu ambazo ziliporwa baada ya tukio na zimetambuliwa na ndugu wa marehemu,” alisema.

Aliwataja waliouawa kuwa ni Mary Charles (42), mwanawe Jenifa Fredy (22) na Monica Jonas (19) aliyekuwa msaidizi wa kazi za ndani wa familia hiyo.

Kwa mujibu wa Kamanda Ng’anzi, chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kibiashara. Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Thomas Songay (26) ambaye ni msukuma mkokoteni, Hajir Thomas (23) fundi cherehani, Deoglas Malengwa (31) muuza duka la vifaa vya umeme na Emmanuel Mathew (19), wote wakazi wa Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana na Emmanuel Lugaila (36) mwendesha mitambo katika mgodi wa Mwadui na anaishi Mecco Kusini wilayani Ilemela.

“Watuhumiwa hawa watafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilisha upelelezi wa tukio hili kwa hatua zaidi za kisheria,” alisema Kamanda Ng’anzi na kuongeza kuwa polisi inaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika kwenye tukio hilo.

Alizitaja mali zilizokamatwa na watuhumiwa hao ni friji moja aina ya Kyoto, godoro, runinga mbili za nchi 18 aina ya Singsung, radio mbili aina ya Seapiano na Alpu, jiko la gesi aina ya Nickle na simu tatu aina ya Tecno zilizopatikana nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa wa maeneo ya Buhongwa.

Kamanda Ng’anzi aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/394ceb101dad371684305eeb77e70940.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi