loader
Majaliwa ataka wazazi washirikiane na walimu kitaaluma

Majaliwa ataka wazazi washirikiane na walimu kitaaluma

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wazazi washirikiane na walimu kuweka mazingira mazuri ya kitaaluma ili wahakikishe watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora

Pia, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya wafuatilie katika maeneo yao ili kuona kama kuna shule zinaendelea kuchangisha michango ambayo iliyozuiliwa na serikali.  

Majaliwa alisema hayo Jumanne alipokagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Babati Day iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara. 

“Wazazi lazima tushirikiane na walimu ili kuhakikisha watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule wanakwenda na ni marufuku kuwakuta wakifanya biashara. Mtoto lazima asome,” alisema Waziri Mkuu.

Alimuagiza mkuu wa wilaya hiyo, Lazaro Twange asimamie maboresho ya madawati katika shule hiyo kwa kuweka mbao badala ya mabati kama ilivyo sasa.

 “Madawati haya si mazuri yarekebishwe ili kuepusha madhara kwa watoto wetu. Marekebisho haya yanatakiwa yafanyike bila kuathiri mwenendo wa masomo kwa wanafunzi,” alieleza.

Aliwaondoa hofu wananchi kuhusu gharama za kuunganishiwa umeme vijijini kwamba itaendelea kuwa Sh 27,000 tu. 

Alisema wananchi hususan waishio vijijini hawahusiki na ongezeko la gharama za kuunganishiwa huduma ya umeme iliyotolewa hivi karibuni na Wizara ya Nishati. 

Alisema malengo ya Serikali ya Awaamu ya Sita ni kuhakikisha vijiji vyote vinapata umeme ifikapo Desemba mwaka huu; hivyo alihimiza wananchi waendelee kufanya maandalizi na malipo kwa ajili ya kuunganishiwa huduma hiyo katika makazi kwani ongezeko hilo haliwahusu. 

Wakati huohuo, Waziri Mkuu aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kusambaza huduma za maji.

Alisema hayo alipozungumza na wananchi katika Kijiji cha Matufa baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Darakuta-Magugu utakaohudumia wananchi zaidi 80,000. 

Mradi huo una uwezo wa kuzalisha lita milioni 5.5 kwa siku, mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 95 na wananchi 45,000 wameanza kunufaika. Mradi huo umegharimu Sh bilioni 3.9.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0394a57da012dc83ea080f17106da6a8.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Babati

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi