loader
Simba, Kagera turufu muhimu

Simba, Kagera turufu muhimu

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wamepania kuivuruga Kagera Sugar katika mchezo wa leo utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.

Mchezo huo awali ulikuwa uchezwe Desemba 18 mwaka jana lakini ukaahirishwa baada ya Simba kuripoti asilimia kubwa ya wachezaji kuugua mafua makali.

Simba inakutana na Kagera ikiwa wametoka kupata pointi moja katika michezo miwili ya ugenini dhidi ya Mbeya City walipoteza bao 1-0 na suluhu dhidi ya Mtibwa Sugar.

Matokeo hayo huenda yakawafanya Simba kucheza kwa presha kuhakikisha wanapambana kupata ushindi ili kurejesha imani ya kutetea ubingwa kwa mashibiki

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kwa namna walivyopata mapokezi makubwa Kagera wachezaji wana deni la kuhakikisha wanapambana na kufanya vizuri.

“Tutawafurahisha mashabiki wetu kwa kuwalipa kile ambacho wametuonesha kwetu,” alisema Ahmed.

Alisema wataingia kwa umakini katika mchezo huo kwani Kagera Sugar ni moja ya timu nzuri lakini wao wanapenda mechi ngumu kwa kuwa zinawajenga kiushindani ila wataonesha ukubwa wao kwa kushinda.

Kocha wa Kagera Sugar, Francis Baraza alisema “tunacheza na timu bora iliyofanya vizuri zaidi ya misimu minne hivyo lazima ujipange  na tumejipanga,”

“Simba wana wachezaji wazuri, benchi zuri, kwa upande wetu tulikuwa na tatizo la ufungaji tumefanyika kazi na kumekuwa na vikao vingi na wachezaji wanajitahidi,”

Iwapo Simba itapoteza au kutoka sare itazidi kujiweka katika presha na kuwapa nafasi zaidi Yanga kuendelea kuongoza kwa tofauti ya pointi nyingi kwani wanatofautiana kwa pointi 10.

Wanacheza na Kagera Sugar ambao walikuwa kwenye nafasi za chini lakini baada ya ushindi katika mchezo uliopita wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji wamesogea hadi nafasi ya 11.

Kagera inapambana kujiondoa chini baada ya kuanza msimu kwa kusuasua na huenda usajili wa dirisha dogo wa kumleta Hamis Kiiza umeanza kuonesha matunda.

Simba itawakosa Jonas Mkude na Kibu Denis ambao ni majeraha lakini kutokuwepo kwao hakutawaathiri kwa kuwa wana wachezaji wengi wazuri.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Mei mwaka jana Simba ilishinda mabao 2-1.

Msimu uliopita zilipokutana katika mizunguko miwili ya ligi na Simba iliondoka na pointi zote sita.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f2d44444ce9792f6069cda884b2af3e0.jpeg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi