loader
TRC kuingiza mabehewa 1,430

TRC kuingiza mabehewa 1,430

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) liko kwenye mchakato wa kuagiza mabehewa 1,430 ya mizigo yakiwemo ya kusafi rishia mafuta na bidhaa ndani na nje ya nchi yatakayotumiwa kwenye Mradi wa Reli ya Kisasa ya (SGR).

Aidha, majaribio ya treni ya SGR kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro yataanza mwishoni mwa Aprili au wiki ya kwanza ya Mei mwaka huu ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa kipande hicho kinachotekelezwa katika mradi huo mkubwa nchini ambao utafika hadi jijini Mwanza.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa wakati akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu ujenzi wa mradi huo nchini.

Kadogosa alisema utekelezaji wa mkataba huo utafanywa hivi karibuni na kusema gharama zake ni Sh bilioni 293.85.

“Tunaagiza mabehewa 1,430 ya mizigo mbalimbali ikiwemo bidhaa na ya kubebea mafuta ambayo yatatumika kusafirishia mafuta nje, hii itasaidia kupunguza msongamano wa magari kule bandarini ya kubeba bidhaa mbalimbali zinazokwenda ndani na nje ya nchi,” alisema Kadogosa.

Aidha, alisema majaribio ya treni ya SGR kipande cha Morogoro -Dodoma yataanza mwishoni mwa Aprili au mwanzoni mwa Mei na kwamba ujenzi wa kipande hicho umekamilika kwa asilimia kubwa.

Kadogosa alisema wakati majaribio hayo yakitarajiwa kuanza, TRC inaendelea pia na mchakato wa ununuzi wa vichwa vya treni za kisasa sambamba na mabehewa ya abiria yatakayotumika kubeba abiria na kufanya pia safari za kitalii kwa kutumia mabehewa maalumu ya ghorofa ambayo yatanunuliwa mabehewa 30 kutoka Ujerumani.

Alisema katika ununuzi huo, wananunua vichwa viwili na mabehewa 30 ambayo yana thamani ya Euro milioni 26.6 na mabehewa mengine 59 yataagizwa kutoka Korea Kusini yatakayotumika kwenye masafa marefu na yana thamani ya Dola milioni 55.

Aidha, TRC pia inaagiza treni 10 na vichwa 17 vya abiria vinavyotumia (EMI) na kuwa kila treni moja itakuwa na uwezo wa kubeba mabehewa nane na treni hizo zitatumika zaidi kwa masuala ya utalii, huku vichwa hivyo 17 vitatumika kwa ajili ya kuvuta mabehewa 59. Alisema vichwa na mabehewa hayo vina gharama ya Dola za Marekani milioni 295.

Katika hatua nyingine, Kadogosa alisema utekelezaji wa mradi huo umekuwa na baadhi ya changamoto zikiwemo mchakato wa kuwalipa fidia wananchi na kulipa viwanda vilivyo jirani na bandari ili kupisha ujenzi wa mradi huo.

Nyingine ni changamoto ya kunyesha kwa mvua kunakokwamisha ujenzi kwenye baadhi ya maeneo na kuchelewa kwa baadhi ya vifaa vya ujenzi vinavyotoka nje ya nchi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/58601c637882e40cdf253f740324514c.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Na Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi