loader
Serikali yavuna bil 122/- Airtel Tanzania

Serikali yavuna bil 122/- Airtel Tanzania

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba ameipongeza Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania kwa mafanikio ya kiuendeshaji na kufanikisha kuipatia serikali zaidi ya Sh bilioni 122 katika kipindi cha miaka miwili.

Dk Mwigulu alitoa pongezi hizo Dodoma alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania aliyemaliza muda wake, George Mathen na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni hiyo, Dinesh Balsingh.

“Fedha hizo zimeiwezesha serikali kutekeleza miradi ya kijamii ambayo imekuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi na kubadilisha maisha yao kama inavyoelekezwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha kuwa kila fedha inayopatikana inaelekezwa kwenye maendeleo ya Watanzania,” alisema Dk Mwigulu.

Aliipongeza Airtel Tanzania kwa kuendelea kuboresha huduma na akatoa mwito kwa kampuni hiyo na kampuni nyingine za simu zitoe maoni kuhusu namna ya kuboresha masuala ya bajeti ya serikali. Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania aliyemaliza muda wake, Mathen alisema katika kipindi chake cha miaka miwili na nusu kuongoza kampuni hiyo, alitoa gawio na malipo mengine kwa serikali yenye thamani ya Sh bilioni 122.

“Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 42 ni gawio kutokana na serikali kumiliki hisa kwenye kampuni, shilingi bilioni 44 ni malipo baada ya kuhamisha umiliki wa minara yake kwenda Kampuni ya Minara pamoja na kiasi kingine cha shilingi bilioni 34 zinazotokana na malipo ya kila mwezi ya shilingi bilioni moja kwa kampuni hiyo ya Minara tangu ilipoingia nayo makubaliano ya kuendesha minara ya mawasiliano kuanzia Aprili mwaka 2019,” alieleza Mathen.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e8694742bb0f31ade49b5f2c1a96647f.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi