loader
‘Mvua zinazonyesha  zitumike kupanda miti’

‘Mvua zinazonyesha zitumike kupanda miti’

WAKUU wa mikoa na wilaya wametakiwa kuhimiza wananchi kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti katika maeneo yao.

Akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa mazingira wa Jiji la Dodoma kutoka sekta binafsi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dk Selemani Jafo alisema ajenda ya mazingira ni ya kitaifa na kuwa wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa kuwahimiza wananchi wao kutumia mvua zinazoendelea kupanda miti katika maeneo yao.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika suala la utunzaji mazingira katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Dk Jafo pia aliwahimiza halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatekeleza agizo la Rais Samia la kuhakikisha kila mwaka wanapanda miti milioni 1.5. Pia aliwataka wananchi kila mmoja kuhakikisha wanapanda angalau miti mitatu.

Hivi karibuni, Ofisi ya Makamu wa Rais, imezindua kampeni ya ‘soma na mti’ yenye lengo la kufanya kila mwanafunzi wa shule na vyuo kupanda mti mmoja na lengo ni kuhakikisha kunapandwa miti milioni 14.5.

Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu, Mazingira, kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Edward Nyamanga alisema kampeni ya kijanisha Dodoma imekuwa ya kusuasua na kuwataka wadau kuhakikisha wanakuja na maazimio ya kufanikisha hilo. Tangu kuanza kutekelezwa kampeni hiyo iliyozinduliwa Desemba 20 mwaka 2017, miti 40,000 imepandwa katika Jiji la Dodoma

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/67e6b2264de8d717adfbaf21bbbba1ba.jpeg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

1 Comments

  • avatar
    Brown
    27/01/2022

    Let's you be serious guy. 400000 trees for capital city from 2017 is a joke to any standard. You can be more innovative by let's say every top government official from directorship to be assigned a road in Dodoma with the responsibility to coordinate and mobilize tree planting in that particular road given. Doing it in free for all fashion will be difficult as there is no specific responsibility to each one of you.

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi