Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema kuna haja ya kuwa na mipango kabambe katika halmashauri zote na sio tu zenye mradi tu.
Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo leo Januari 27, 2022 wakati akipokea taarifa ya miradi ya Tscp, Ulgsp na Dmdp kutoka kwa kikundi kazi kinachosimamia miradi inayotekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia Tarura.
“Nimesikia kuwa Mpango Kabambe (Master Plan) imeandaliwa kwenye Halmsahuri zilizonifaika na mradi tu kwenye miji 18, majiji na manispaa pamoja na halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam lakini kwa namna miji yetu inavyokua kwa kasi Mpango Kabambe inatakiwa kuandaliwa kwenye halmashauri zote,” amesema Bashungwa.
Waziri Bashungwa yupo ziarani Jijini Dar es salaam kukagua utekelezaji wa mradi wa Mabasi yaendayo haraka na Miradi inayotekelezwa chini ya fedha za mkopo toka Benki ya Dunia