loader
CCBRT yapokea msaada

CCBRT yapokea msaada

HOSPITALI ya CCBRT imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Taasisi ya RYTHM Foundation Tanzania.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo leo, Mkuu wa Kitengo cha Uuguzi Emelda Lwena, ameshukuru na kusema msaada huo wa mashuka, taulo za kike, shani, sukari, vijiko, neti pamoja na vitu vingine ambavyo ni muhimu katika jitihada za hospitali hiyo kuhudumia watu na kubadili maisha yao.

Ameeleza kuwa tangu mwaka 2003, CCBRT imefanya zaidi ya upasuaji 10,000 kwa wanawake wenye fistula bila malipo.

“Tangu 2003, CCBRT iliondoa gharama zote za matibabu kwa wagonjwa wa fistula, kwa kufanya hivyo tumeweza kuondoa kikwazo kikubwa kwa wagonjwa wengi ambao wasingeweza kupata matibabu.”

Lwena amesema “kwa niaba ya CCBRT, ningependa kuishukuru taasisi ya RHYTHM  kwa msaada wenu na ukarimu, hii imedhihirisha kujitoa kwenu katika kazi hii ya kubadili maisha ya watu. Tunatiwa moyo na watu mbalimbali wenye moyo wa ukarimu na wakujitolea kama wenu.”

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja wa QNET Ukanda wa Kusini mwa Afrika, Biram Fall, amesema msaada huo umelenga kufikia jamii ya watu ambao wamesahaulika na wenye uhitaji sambamba na falsafa ya kampuni ya RYTHM yenye kauli mbiu ‘Jiinue Ili Kumsaidia Mwanadamu’.

Ameongeza kuwa msaada huo pia unaakisi matakwa ya kampuni ya ushirikiano katika maswala ya kijamii na kuleta matokea chanya.

“Umaskini unawaweka watu katika hatari ya kupata maambukizi mbalimbali na kuwaathiri sana,” ameeleza.

Amesema kutokana na janga la Covid-19, watu wengi wamepoteza vyanzo vyao vya kujipatia kipato na wanaishi kwa mashaka makubwa.

“Tumefanya kidogo tunachoweza kurudisha tabasamu na furaha kwa wale wanaohitaji zaidi,” ameeleza Fall.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fdaf9d38f17b271d366fa37b84498606.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Bernard Lugongo

1 Comments

  • avatar
    Otto Amos
    28/01/2022

    Keep working together as a team, keep showing more hospitality to other people who needs help.

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi