loader
Niliitwa Bibi Mchele – Rais Samia

Niliitwa Bibi Mchele – Rais Samia

RAIS  Samia Suluhu (62) ametoboa siri ya kumpa ushindi mara baada ya kuingia kwenye siasa ni jina la Bibi Mchele ambalo alipewa na wananchi wakati akifanya kazi kwenye Shirika la Chakula Duniani (WFP).

Katika mahojiano maalum ya Jambo Tanzania kupitia televisheni ya Taifa ya TBC yaliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma leo, amesema jina hilo lilimpa umaarufu mkubwa na ndio lilimfanya kukubalika kirahisi alipojitosa kwenye siasa.

 “Nilikuwa sijui mtu anaingiaje kwenye siasa, nikauliza nikafahamishwa nikajaribu, nikaenda Kusini ya Unguja nikajitambulisha wengi walikuwa wananijua kwa jina la Bibi Mchele kwa sababu wakati nafanya kazi Shirika la Chakula Duniani (WFP) kulikuwa na tatizo la wadudu kuvamia mazao, kwa hiyo kukawa na uhaba wa chakula lakini kwa sababu niko kule nikafanya jitihada za kuomba chakula kwa ajili ya wananchi”

“Tukapata mchele, samaki na mafuta ya kupikia kwa wingi tukagawa kwa wananchi, kwa hiyo wakanipa jina la bibi mchale, nilipokwenda kujitambulisha wakawa wanasema bibi mchele tunampa, kwa hiyo nikaibuka kuwa mshindi kwenye viti vya wanawake ndio nilipenyea huko”anasema

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a32894b8708393ccef7cfc12cd79ac12.jpg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi