NAIBU Waziri wa Kilimo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini , Anthony Mavunde ametembelea Kata ya Nzuguni kukagua ujenzi wa daraja la Nzuguni B ambao umesimama kupisha mvua.
Mavunde amewataka Wakala wa Barabarani Vijijini na Mijini (TARURA) kushirikiana na mkandarasi kukamilisha mapema ujenzi wa daraja hilo na wahakikishe wanaboresha njia za mchepuko ili zipitike kwa urahisi na kuwapunguzia adha wananchi wa eneo hilo..
Katika ziara hiyo fupi, Mavunde aliongozana na Mameneja wa TARURA wa mkoa na wilaya,wenyeviti wa mitaa na Diwani wa Kata ya Nzuguni Alloyce Luhega.
Awali Luhega ambaye ni diwani wa kata hiyo akiwasilisha changamoto za eneo hilo amesema barabara za eneo hilo zimekuwa kero kwa wananchi hususani kipindi cha mvua na kutaka uwarakishwaji katika ujenzi wa barabara hiyo ili kuwaondolea wananchi adh na kupunguza usumbufu hasa kwa wanafunzi wa shule..