RAIS wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi, amefanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za Taasisi za Umma ambapo amemteua Dk Said Seif Mzee kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.
Katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A. Said imesema Rais Dk Mwinyi pia amemteua Salim Mahfoudh kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango katika ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.
Aidha Rais Mwinyi amemteua Akif Ali Khamis kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi huku CDR Mohamed Khamis Makame akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Meli Zanzibar katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.
Taarifa hiyo imesema, uteuzi huo umeanza leo Januari 27, 2022.