loader
Bashungwa awataka wakuu wa Mikoa kusimamia usafi

Bashungwa awataka wakuu wa Mikoa kusimamia usafi

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi, Innocent Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa  pamoja na Wakuu wa Wilaya zote nchini kuhakikisha wanasimamia suala zima la usafi hususani katika miradi yote ya barabara, masoko na stendi inayoendelea kujengwa katika maeneo yao.

Bashungwa amesema mkoani Dar es Salaam wakati akipokea taarifa ya miradi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa kuendeleza Miji Mkakati (TSCP) mradi wa Ukuzaji na Uboreshaji wa Miji (ULGSP) na Mradi wa Uboreshaji na Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam(DMDP) kutoka kwa kikosi kazi kinachosimamia miradi hiyo inayotekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia na kusimamiwa na Wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA).

Alisema haipendezi kuona barabara, masoko na stendi zilizojengwa kwa gharama kubwa tena kwa fedha za Serikali zikiwa chafu huku akitaka elimu iendelee kutolewa zaidi kwa wananchi hatua itakayosaidia kuondokana na tatizo hilo.

Waziri Bashungwa yupo ziarani Jijini Dar es salaam ambapo juzi alitembelea na kukagua utekelezaji wa miradi zikiwemo barabara, ujenzi wa daraja la juu eneo la Magomeni, pamoja na Mto Msimbazi eneo la Jangwani.

Aidha akiwa mahali hapo Waziri Bashungwa alisisitiza adhma ya Serikali kujenga daraja la juu litakaloanzia eneo la Magomeni hadi 'Fire' na kusema kuwa ujenzi wake utasaidia changamoto iiloyopo eneo hilo hususani mafuriko hasa nyakati za mvua.

Waziri Bashungwa alifaanya ziara katika Ofisi ya Mabasi yaendayo haraka (DART)  kwa lengo la kujionea maendeleo ya taasisi hiyo sambamba na kufahamu changamoto zake akitumia fursa hiyo pia kutembelea miundombinu inayotoa huduma na ile inayoendelea kujengwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9bbe884840771207bba2a77e1f3720e4.jpeg

MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi