loader
ACT Wazalendo yaunda Baraza mawaziri kivuli

ACT Wazalendo yaunda Baraza mawaziri kivuli

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeunda baraza kivuli la mawaziri lenye wizara 24.

Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe alisema jana kwamba baraza hilo litafanya kazi zake nje ya Bunge na wengi ni vijana na kwamba limezingatia taaluma za walioteuliwa.

Zitto alisema hayo Dar es Salaam alipozungumza na wahariri na waandishi wa habari.

Alisema chama hicho kimeunda baraza hilo kivuli kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 yaliyokifanya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua takribani viti vyote vya ubunge hivyo vyama vya upinzani haviwezi kuunda Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

“Matokeo ya Uchaguzi Mkuu yalisababisha kurudisha nyuma nchi yetu katika ujenzi wa demokrasia ya vyama vingi na hivyo kuathiri sehemu kubwa ya mfumo mzima wa kuiwajibisha serikali na vyama kutoa mawazo mbadala ya kisera kwa wananchi,” alidai Zitto Kabwe.

Alisema dhana hiyo huitwa Baraza Kivuli la Mawaziri lakini kwa kuwa wameamua kufanya kazi hiyo nje ya Bunge, wameamua kuiita Kamati ya Kuisimamia Serikali ambayo inaundwa na wasemaji wa kisekta watakaokuwa na wajibu wa kutoa sera mbadala.

“Kila sekta itasaidiwa na sekretarieti ambayo itafanya tafiti na kuzalisha sera mbadala, kwa njia hii tutaweza kufanya kazi kwa wananchi na kuwa wasemaji wao, kuibua masuala muhimu ya wananchi, kuyatolea mapendekezo na majawabu ya mapendekezo hayo,” alisema.

Zito aliwataja wateule hao na wizara zao katika mabano kuwa ni Dorothy Semu (Waziri Mkuu), Abdul Nondo (Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Baraza), Emanuel Mvula (Fedha na Uchumi), Fatma A. Ferej (Mambo ya Nje), Masoud Abdallah Salim (Ulinzi) na Mbarala Maharagande (Mambo ya Ndani).

Wengine ni Mama Riziki Shahari Mngwali (Elimu), Dk Nasra Omar (Afya), Mwanaisha Mndeme (Uwekezaji Mashirika ya Umma na Hifadhi ya Jamii), Pavu Juma Abdallah (Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Muungano), Kulthum Mchuchuli (TAMISEMI na Maendeleo ya Jamii), Isihaka Mchinjita (Nishati) na Edgar Mkosamali (Madini).

Zitto aliwataja wengine kuwa ni Halima Nabalanganya (Viwanda na Maendeleo ya Biashara), Esther Thomas (Maji na Mazingira), Wakili Victor Kweka (Katiba na Sheria), Mtutura Mtutura (Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Bonoifasia Mapunda (Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

Sekta zingine zilizotajwa ni panmoja na miundombinu ya ujenzi, barabara na reli chini ya Mhandisi Mohammedi Mtambo. Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Uchukuzi itakayoongozwa na Ally Saleh, Maliasili na Utalii chini ya Juliana Mwakang’wali, na Utamaduni, Sanaa, Ubunifu na Michezo chini ya Webiro Wassira.

Sekta zingine ni Vijana, Kazi na ajira itakayoongozwa na Mwalimu Philbert Macheyeki sambamba na Ustawi na Maendele ya Jamii, Wanawake na Watoto.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/77ce7c955559069f728693682808a13f.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi