“SIKU kama ya leo mimi mwenzenu tangu asubuhi nasikia sauti ya mtangulizi wangu Dk John Magufuli na maono yake ya kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu, nami nawaahidi tunakwenda kukamilisha mradi huu kama alivyotaka uwe.” amesema Rais Samia Suluhu, leo Februari 9, 2022, akiweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3.
Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa kilomita 52.3 kupitia Nala, Veyula, Mtumba na Ihumwa na awamu ya pili itahusisha kilomita 60 kupitia Ihumwa, Matumbulu hadi Nala.
Barabara hiyo itafungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa Dodoma sanjari na kuondoa msongamano wa magari yanayokwenda mikoa mingine.
“Barabara hii inakwenda kutupeleka kwenye masoko ya mazao yetu ya kilimo lakini pia bidhaa za viwandani pia itatufungulia masoko ili Tanzania tuweze kuzalisha zaidi na tujenge uchumi zaidi na zaidi.” amesema Rais Samia na kuongeza
“Mategemeo yetu ni kwamba mikoa ya jirani kama Singida, Manyara, Morogoro na Iringa itanufaika zaidi lakini pia Kanda hizi za Afrika ambazo tupo karibu nazo na majirani zetu tunakwenda kuunganishwa nao wote kupitia barabara hii,” amesisitiza
Kwa upande wa Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Dk Akinwumi Adesina amempongeza Rais Samia kuwa rais wa kwanza mwanamke Tanzania na kwamba hiyo ni fahari si tu kwa Tanzania bali pia kwa Afrika kwani mwanamke akishinda Afrika imeshinda.
“Nakupongeza kwa kuchukua nafasi ya Hayati kaka yangu na rafiki yangu John Magufuli, na kuendeleza kazi kubwa aliyoaicha na kutekeleza ndoto ya Tanzania kukuwa kiuchumi.” amesema Dk Adesina na kuongeza
Mara zote unasema ‘Nakusalimu kwa jina la Muungano wa Tanzania,..Kazi iendelee’
Aidha amesema ujenzi wabarabara hiyo itakuwa kiunganishi kwa nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Demokrasia ya Congo.
Amesema mahusiano mema kati ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na Tanzania, benki hiyo itaendelea kusapoti maoni ya Tanzania 2025 na kwamba benki hiyo imewekeza Dola bilioni 2.5 kwa ajili ya mradi wa kiwanja cha ndege cha Msalato Dodoma, barabara ya Bagamoyo hadi Horohoro, Kasulu – Nyakanazi, Neivata hadi Newala Masasi.
“Benki ya Maendeleo Afrika ipo pamoja na watanzania na kuhakikisha Tanzania inaendelea kung’aa,” amesema