loader
Australia yaitaka China  kuondoa

Australia yaitaka China kuondoa "ukimya" ukraine

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison ametoa wito kwa China kukomesha "ukimya wake" juu ya mashambulio ya Urusi huko Ukraine, akisema kwamba "hakuna nchi yoyote duniani itakuwa kubwa" katika kumaliza mzozo huo.

Akiongea katika Taasisi ya Lowy huko Sydney siku ya Jumatatu, Morrison alionya kwamba, bila Beijing kulaani moja kwa moja vitendo vya Moscow, ulimwengu una hatari ya kubadilishwa na "utawala wa kiimla" kutokana na uhusiano wa China na Urusi.

"Nilikuwa nikisikiliza sauti ya serikali ya China ikiwa italaani vitendo vya Urusi lakini kulikuwa na ukimya wa kutisha," alisema Morrison.

"China imedai kwa muda mrefu kama moja ya mataifa makubwa duniani na yenye jukumu lakuchangia amani na utulivu," Waziri Mkuu aliongeza, akiitaka Beijing kujitokeza na kuchukua hatua wakati mzozo wa Ukraine ukionekana kuongezeka.

Morrison alidai kwamba mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine hayaendi kama ilivyopangwa, akidai Kremlin "imekadiria uwezo" wa jinsi inaweza kutimiza malengo yake ya kijeshi.

Ukosoaji huo kutoka kwa Morrison unakuja licha ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi kudai Jumatatu kwamba Beijing iko tayari kuwezesha mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5ec77337366bf681d980180ea6541a62.jpg

RAIS Mstaafu wa Awamu ya ...

foto
Mwandishi: Canberra ,Australia

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi