loader
Serikali yaeleza mafanikio vita ya Ukimwi

Serikali yaeleza mafanikio vita ya Ukimwi

SERIKALI imesema imepiga hatua kubwa katika kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini kwa kutelekeza programu mbalimbali za utoaji elimu na huduma kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, Balozi Dk. Pindi Chana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, akitoa taarifa ya mafanikio ya Ofisi yake katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema  miongoni mwa hatua kubwa zilizopigwa na serikali ni pamoja na kudhibiti vifo vitokanavyo na Ukimwi, ambapo vimepungua  kwa asilimia 50  kutoka 64,000 mwaka 2010, hadi 32,000 mwaka 2021.

“Katika kipindi  cha mwaka mmoja mafanikio ya Serikali yaliyoshuhudiwa katika eneo hili ni kupungua kwa kiwango cha maambukizi mapya ya VVU katika jamii, ikiwemo maambukizi mapya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kushuka kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia 7 mwaka 2021,”alisema Waziri huyo.

Akibainisha mafanikio mengine katika mapambano dhidi ya Ukimwi, alisema ni kushuka kwa kiwango cha unyanyapaa katika jamii kutoka asilimia 28 mwaka 2013, hadi asilimia 5.5 mwaka 2021.

“WAVIU wanaofahamu hali zao za mambukizi ni asilimia 83, WAVIU wanaofahamu hali zao za mambukizi na wapo kwenye matibabu ni asilimia 98 na WAVIU waliopo kwenye matibabu na wamefubaza VVU ni asilimia 92,”alieleza Waziri Pindi.

Pia akitaja mafanikio mengine ya Serikali ya Awamu ya Sita alifafanua kuwa ni pamoja na Uzinduzi wa ujenzi wa majengo ya Ofisi za Wizara na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mji wa Serikali, ambao unaendelea na ukitarajiwa kukamilika mwaka 2022/23.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/aed9c7ed155f0bd9db71b3b568464064.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi