loader
Samia atoa maagizo akiwaapisha Polepole, Kindamba

Samia atoa maagizo akiwaapisha Polepole, Kindamba

RAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba atafute mbinu ya kukuza kipato cha wananchi katika mkoa huo.

Pia amemuagiza asimamie suala la lishe kwa wananchi kwenye mkoa huo kwa maelezo kwamba ingawa Mkoa wa Njombe una kila kitu bado kuna tatizo la utapiamlo.

Rais Samia alisema hayo jana katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma katika hafla ya kuwaapisha Hamphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi na Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Alisema anafikiria kuingia mikataba na wakuu wa mikoa kuhusu usimamizi wa suala la lishe katika mikoa yote nchini akisema mikataba ya awali aliyoingia na viongozi hao wa mikoa ilikuwa ya mafanikio kwa kuwa walifanya vizuri.

Rais Samia alimuagiza Kindamba asimamie suala la chanjo kwa wananchi katika mkoa huo kwa kuwa kuna kirusi kipya cha corona aina ya Omicron namba mbili ambacho kimeripotiwa katika mataifa ya Asia.

“Usisahau suala la chanjo, nenda jitahidi shirikiana na wenzio kahamasishe watu wachanje kama mlivyosikia tayari kuna Omicron B01 ameanza huko Asia na wakianza huko hawako mbali kuja kwetu, kwa hiyo naomba mkasimamie hilo,” alisema Rais Samia.

Alisema Polepole atapatiwa mafunzo katika Chuo cha Diplomasia na kabla hajaondoka kwenda Malawi atakutana naye wazungumze.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema kitendo cha kuteuliwa kwa viongozi hao ni ishara kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anawaamini na ana mategemeo makubwa kwao na Watanzania wana mategemeo makubwa kwao kupitia utendaji wao mahali walikotoka.

“Mkuu wa Mkoa wewe ni kiongozi wa serikali katika mkoa wako, Njombe ni mkoa uliojipambanua kwa shughuli za kiuchumi nyingi ikiwemo kilimo lakini pia shughuli mbalimbali za ujasiriamali na shughuli zingine ambazo Wananjombe wanashughulika nazo,” alisema Majaliwa

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/903399743beb66e5a4b45c32939420e5.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Selemani Nzaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi