loader
‘Simamieni upatikanaji taarifa sahihi walioacha shule’

‘Simamieni upatikanaji taarifa sahihi walioacha shule’

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, David Silinde amewataka Maofisa Elimu Watu Wazima wa Mikoa na Halmashauri kusimamia upatikanaji wa taarifa sahihi za wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali, ili waweze kurudi shuleni.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kufungua Mkutano wa Mafunzo Elekezi yanayolenga kuboresha utoaji wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi, lengo likiwa ni kujifunza na namna ya kuzitatua changamoto za elimu.

Naibu Waziri Silinde amewataka wasimamizi wa elimu ya watu wazima kufanya kazi kwa weledi, ili nafasi iliyotolewa na serikali  kwa wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali waweze kurudi shule kuendelea na masomo.

Amesema serikali inatambua kuwa jamii iliyoelimika, yenye maarifa, ujuzi na uzalendo ndio msingi wa maendeleo ya ujengaji wa uchumi hasa ujenzi wa uchumi wa viwanda.

“Haya ni sababu ya usimamizi mzuri wa elimu ya awali, msingi sekondari na elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi,” amesema Silinde.

“Serikali inaendelea kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia, ili kupata idadi kamili ya walengwa wa elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi, ninawaelekeza fuatilieni upatikanaji sahihi wa takwimu  za elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi kwa kuendelea kuutumia mfumo wa BEMIS,” amesema Naibu Waziri huyo.

Pia amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmshauri zote, kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi na kuzisimamia utekelezaji wake.

Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Gerald Mweli amewataka viongozi hao kuendelea kusimamia na kufuatilia wanafunzi wote walioacha shule kwa sababu mbalimbali.

Amesema mpaka sasa takwimu zinaonesha zaidi ya wanafunzi 909 wamesharudi shule kuendelea na masomo, kati ya hao wapo wenye sababu mbalimbali zikiwemo utoro na ujauzito.

Naye Ofisa Elimu Watu Wazima, Martha Ignatus, ameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya watumishi na kuahidi maelekezo yote wanaenda kuyafanyia kazi.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/98520230b0a5957175c07a9dfe828873.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi