loader
Majaliwa afagilia mafanikio michezoni

Majaliwa afagilia mafanikio michezoni

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amezindua Mkakati wa Maendeleo ya Michezo, wakati alipofungua rasmi Kikao kazi cha Maofisa Utamaduni na Michezo, huku akipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mafanikio yaliyopatikana katika kipindi hiki kutokana na mikakati madhubuti iliyojiwekea.

 Amesema kuwa Wizara ya Utamaduni,  Sanaa na Michezo inafanya kazi kubwa, ambayo imekuwa na mchango mkubwa kwa pato la taifa, utulivu wa nchi na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

"Kazi kubwa mnayoifanya inaleta furaha ndani ya mioyo yetu. Sifa ya nchi yetu ambayo ipo ndani na nje imetokana na umoja, utulivu na amani na mshikamano tulionao,” amesema Waziri Mkuu.

Amesema sekta ya sanaa imeweza kuitangaza Tanzania na kwamba nchi imepata heshima kubwa kutokana na michezo mbalimbali kufanya vizuri, huku akitolea mfano wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya walemavu ‘Tembo Warriors’, ambayo imefuzu michuano ya Kombe la Dunia la mchezo huo.

 

 “Hadi ninapozungumza sasa, tayari wachezaji wanne wa timu yetu ya Tembo Warriors wamesajiliwa kwenye timu za kimataifa katika mataifa ya nje, ukiachilia mbali michezo mingine kama ngumi, kuogelea ambayo pia inafanya vizuri sana,” amesema Waziri Mkuu.

 Amesema Tanzania imepiga hatua kufika uchumi wa kati, ambapo amesema sekta ya sanaa ina mchango mkubwa katika hilo na kusisitiza kuwa huwezi kutenganisha utamaduni na maendeleo yaliyofikiwa hivi sasa hapa nchini.

 Ametumia kikao hicho kutoa maelekezo mbalimbali ya serikali  kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na wizara nyingine kwenye eneo la utamaduni na michezo,  ili kuleta maendeleo katika sekta hizo.

Akimkaribisha Waziri Mkuu kutoa hotuba yake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewashukuru viongozi wakuu wa nchi kwa kutoa kipaumbele kwenye sekta anazoziongoza, huku akisema sekta za michezo na sanaa zina mchango mkubwa kwa taifa.

Amesema sekta hizo zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzalisha ajira rasmi na zisizo rasmi, zinachangia kuimarisha afya za wananchi kupitia  mazoezi,  hivyo kupunguza magonjwa yasiyoambukiza, kukuza utalii na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c6bf22c600c792746d0a2d1fb3dbf970.jpg

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: John Mapepele

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi