loader
Korea Kaskazini yarusha kombora lingine

Korea Kaskazini yarusha kombora lingine

KOREA Kaskazini imerusha kombora la balestiki kutoka katika nyambizi, ambalo liliruka zaidi ya Kilometa 600 na kutua baharini.
Uzinduzi huo umekuja siku tatu baada ya kushindwa kwa jaribio la kombora la masafa marefu, siku chache kabla ya kuapishwa kwa Rais wa Korea Kusini Yoon Seok-youl.
Korea Kaskazini ilirusha kombora la masafa mafupi kutoka katika maji ya Sinpo katika mji wa Hamgyong Kusini hadi Bahari ya Mashariki na liliruka mwinuko wa kilomita 60.
Kombora hilo huenda likawa toleo lililoboreshwa la kombora la KN-23 Iskander na linaonekana kuwa na uwezo wa kubeba vichwa vya kivita vya nyuklia.
Katika muda wa miezi minne iliyopita, Korea Kaskazini imerusha zaidi ya makombora 20 mara 15 au karibu mara moja kwa wiki. Mengi yanaonekana kulenga Korea Kusini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/432086e31343ef0d02928e0cf66eb5ab.jpg

Papa Francis amesema anatarajia kuzuru Ukraine lakini anasubiri ...

foto
Mwandishi: Pyongyang, Korea

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi