loader
Viongozi duniani walaani mauaji ya mwandishi wa Al Jazeera

Viongozi duniani walaani mauaji ya mwandishi wa Al Jazeera

Marekani na Umoja wa mataifa zimelaani vikali mauaji ya mwandishi wa habari wa Al Jazeera ambaye alikuwa anaripoti kuhusu operesheni ya jeshi la Israel katika ukingo wa magharibi katika mji wa Jenin.

Shireen Abu Akleh ambaye ni raia wa Marekani mwenye asili ya Palestina mwenye umri wa miaka 51, alipigwa risasi licha ya kuripotiwa kutambulika vyema kama mwandishi wa habari kutokana na kuvaa nguo zinazomtambulisha kuwa ni mwandishi wa habari.

“Tumeshtushwa na mauaji ya mwanahabari raia wa Marekani, Shireen Abu Akleh katika ukingo wa Magharibi na tunalaani vikali mauaji hayo,” alisema Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani,  Ned Price ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

“Uchunguzi lazima ufanyike haraka na uwe wa kina na waliohusika wawajibishwe. Kifo chake ni shambulio kwa uhuru wa vyombo vya habari kila mahali duniani,” aliongeza Price.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imeandika kwenye Twitter kuwa imeskitishwa sana na mauaji hayo. “Ofisi yetu iko uwanjani kuthibitisha ukweli. Tunaomba uchunguzi huru na wa wazi kuhusu mauaji yake. Tabia ya kutoadhibu lazima ikomeshwe.” Ilisema taarifa ya Ofisi ya Haki za Binadamu.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas na Al Jazeera wameelezea kifo cha Abu Akleh kama mauaji ya kinyama yaliyofanywa na jeshi la Israel, ambalo lilisema darzeni ya Wapalestina wenye silaha walikabiliana na wanajeshi ambao walimkamata mwanamgamo wa kundi la Hamas mjini Jenin.

Waziri mkuu wa Israel Naftali Bennet amesema Abbas ametoa madai yasiyokuwa na msingi hata kabla ya uchunguzi wa kina kufanyika juu ya tukio hilo. “Inaonekana Wapalestina wenye silaha ambao walikuwa wanafyatua risasi kiholela wakati huo walihusika na kifo cha kuskitisha cha mwanahabari huyo,” Bennet alisema katika taarifa.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema mauaji hayo hayakubaliki katika dunia inayothamini na kupigania uhuru wa habari na kuongeza kuwa uchunguzi huru unatakiwa ili kubaini sababu ya kifo cha mwandishi huyo.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeu alisema kitendo kilichofanywa na Jeshi la Israel hakikubaliki na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa dhiudi ya wote waliohusika kutenda uhalifu huo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/863df6c535f5f1d4fb539fa4dab66ed3.jpg

Papa Francis amesema anatarajia kuzuru Ukraine lakini anasubiri ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi