loader
Majaliwa atoa maelekezo wanafunzi waliorejea kisa vita

Majaliwa atoa maelekezo wanafunzi waliorejea kisa vita

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi waliokuwa wakisoma katika vyuo vya elimu ya juu nje ya nchi waripoti katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ili iweze kurasmisha taaluma zao kwa hapa nchini.

Akijibu swali la Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro, Saashisha Mafuwe (CCM), Majaliwa amesema wanafunzi ambao walikuwa wakisoma katika vyuo ambavyo havikidhi viwango vya Tanzania watapewa ushauri wa kozi mpya za kusoma.

“Niwatake wanafunzi wote waripoti TCU ili ifanye ulinganifu wa kozi walizokuwa wakisoma na kozi zilizopo nchini katika vyuo vya ndani ili kuondoa tatizo lililopo,” amesema Waziri Mkuu.

Awali Mbunge alihoji mpango wa serikali juu ya wananchi wakiwemo wanafunzi waliorejea nchini kufuatia kuibuka kwa janga la UVIKO-19 na vita vya Ukraine ambapo walilazimika kukatisha masomo yao na wachache wamekuwa wakisoma kwa njia ya mtandao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5823db4599220982a227b597d96372c8.png

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi