MSANII wa bongo fleva, Hamisa Mobeto, amesema kazi zake hazihusiani na watoto wake, ndio mana amepunguza hata kuwarusha mitandaoni.
Amesema kutokana na hali hiyo kama kuna mtu anataka kufanya jambo kwenye maisha kuhusu yeye, asiwahusishe watoto wake, maana hawahusiki.
"Ukitaka kufanya kitu chochote kinachonihusu Hamisa naomba usihusishe mwanangu wala familia yangu, ndio maana hata nimepunguza kuwaweka mitandaoni, nikiweka labda siku yao kuzaliwa," amesema Hamisa.