MSANII wa bongo fleva, Lulu Euggen, 'Amber Lulu' amesema huu si wakati sasa wa kuweka picha zisizo za kimaadili mitandaoni kwa nia ya kusaka umaarufu, bali ni wakati wa kufanya kazi.
"Nilikuwa nikifanya makosa kuacha mwili wangu wazi, lakini sasa akili yangu imepanuka na nina mtoto anayenitegemea kwa kila kitu, hivyo sitaki kusikia mambo hayo tena kwenye maisha yangu.
“Kujiachia sehemu kubwa ya mwili kwa sasa ni ushamba na vitu hivyo vimepitwa na wakati kwa sababu hata mimi najilaumu sana.
“Mimi ni mama sasa na najitambua na ninataka mtoto wangu aige mfano mzuri kutoka kwangu,” anasema Amber Lulu.