SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), kati ya Yanga na Simba utafanyika Mei 28, 2022 mjini Mwanza.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa muda mfupi uliopita, unaonesha kuwa mchezo huo utaanza saa 9 alasiri Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo mwingine wa Nusu Fainali kati ya Azam FC na Coastal Union utafanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha Mei 29 mwaka huu na fainali ya michuano hiyo itafanyika kwenye uwanja huohuo, Julai, 2, 2022.