loader
Balozi afurahia  malori ya Uganda  Tanzania

Balozi afurahia malori ya Uganda Tanzania

BALOZI wa Tanzania nchini Uganda, Dk Aziz Mlima, amesema moja ya faida kubwa za kiuchumi kutokana na ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Uganda, ni kurejea kwa malori ya Uganda katika kutumia Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema hatua hiyo inakuja baada ya Tanzania kushusha gharama za tozo kwa malori yanayotumia Bandari ya Dar es Salaam kutoka Dola za Marekani 16 kwa kilometa 100 hadi Dola 10. Ada hii mpya itakuwa nafuu kwa Uganda na itarahisisha shughuli za kibiashara kati ya Tanzania na Uganda ambalo ni taifa lisilo na bahari.

Taifa hilo limekuwa likitumia Bandari ya Dar es Salaam kuingiza mizigo nchini kwake. Kwa mujibu wa balozi huyo, Rais Samia alitangaza kuondoa kikwazo hicho kisicho cha forodha kwa malori yanayotumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Mwaka wa Fedha wa 2022/2023 unaoanza Julai Mosi.

“Hii ina maana ya kuwa Uganda sasa malori yake hayatatofautiana sana au yatakuwa sawa malipo ya tozo ya matumizi ya barabara na nchi za Rwanda na Burundi; tozo mpya kwa Uganda itakuwa Dola 10 kwa kila kilometa 100,” alisema.

Balozi Mlima alisema kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha kutakuza biashara na shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizi hali itakayoongeza fursa mbalimbali za kibiashara na kukuza pato katika mataifa hayo.

“Hali hii itaongeza idadi ya usafiri wa malori kutoka Uganda yatakayotumia barabara za Tanzania na hivyo kuleta nafuu kwa wafanyabiashara. Kimsingi, ilikuwa ziara nzuri yenye tija kubwa na ya mafanikio tele,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/78a2d8b7b40668374269cc3e2a38fcd1.jpg

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Adam ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi