SHUGHULI ya ugawaji wa pembejeo za korosho imezinduliwa rasmi mkoani Mtwara kwa msimu wa korosho 2022/2023.
Uzinduzi huo wa viuatifu vya zao hilo la korosho umefanyika leo Mei 17, 2022 kwa mikoa yote inayolima korosho nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Marco Gaguti amevitaka vyama vikuu pamoja na vyama vya msingi kuweka kumbukumbu sahihi ya idadi ya viuatilifu, ambavyo vitapelekwa kwa wakulima wa zao hilo.