loader
Vijana wajitolea kuhamasisha sensa Mwanza

Vijana wajitolea kuhamasisha sensa Mwanza

ZAIDI ya vijana 100 mkoani Mwanza, wameunda umoja wa mabalozi wa sensa wa kujitolea kwa ajili ya kusaidia tukio la sensa lipate matokeo chanya.

Wakitangaza mikakati yao jijini Mwanza, leo Mei 17, 2022, Mwenyekiti wa umoja huo, Mansour Jumanne amesema wameguswa na umuhimu wa  sense, kwani ina faida kubwa kwa maendeleo ya Taifa.

Mwenyekiti huyo aliitaka jamii ihamasike na kutoa ushirikiano mkubwa kwa suala la sense, ili taifa liweze kupata takwimu ya idadi ya watu  na kupanga mipango ya maendeleo.

Amesema mabalozi hao watatumia mbinu mbalimbali, ikiwemo uhamasishaji kwa njia ya nyimbo, ujumbe wa hamasa na sanaa mbalimbali.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana, Boniphace Boniphace, amesema wamehamasika kwa ajili ya umuhimu wake kwa taifa, akisema wanataka kusaidia kusukuma mbele juhudi za serikali kufanikisha kazi hiyo.

Umoja huo unaundwa na vijana wa kada tofauti waandishi habari, wanafunzi wa vyuo vikuu, wasanii, wanasheria, waganga na wauguzi.

foto
Mwandishi: Suleiman Shagata, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi