loader
Wadau wafagilia maboresho bandari Tanga

Wadau wafagilia maboresho bandari Tanga

WADAU wa bandari nchini, wamesema kuwa maboresho ya miundombinu yanayofanywa katika bandari ya Tanga yatasaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kuongeza mapato.

Pia wamesema yatasaidia kupunguza msongamano katika bandari ya Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na wadau hao wakati wa ziara waliyoifanya ya kujionea ujenzi wa mradi wa gati yenye urefu wa meta 450, pamoja na vifaa vya kisasa vya upakuaji wa shehena ya mizigo kwenye bandari ya Tanga.

Mkurugenzi wa huduma za Uchukuzi Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka, amesema kuwa maboresho hayo yanalenga uwezo wa kuhudumia shehena ya mizigo hadi kufikia tani milioni tatu.

Awali Meneja wa Bandari ya Tanga, Mhandisi Masoud Mrisha alisema mradi huo, ambao upo awamu ya pili ya utekelezwaji wake umfikia asilimia 45 na utarajiwa kukabidhiwa Novemba mwaka huu utakaokuwa na meta 450

foto
Mwandishi: Amina Omary, Tanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi