Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, leo Mei 17, 2022, amekutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Reverien Ndikuriyo.
Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Katibu Mkuu, Chongolo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam.