loader
‘ Waandishi tumieni changamoto za kidigitali kuwa fursa’

‘ Waandishi tumieni changamoto za kidigitali kuwa fursa’

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora  ametoa wito kwa waandishi wa habari mkoani Kagera kuzibadili changamoto za kidigitali zilizopo kuwa fursa.

Amesema changamoto hizo wasipozichukulia kama fursa wataona ni kitu kigeni katika utendaji wao wa kila siku.

Prof. Kamzora ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho  ya siku ya Uhuru wa vyombo  habari mkoani Kagera,  amesema anatambua baadhi ya waliosoma taalum ya uandishi wa habari miaka ya zamani, wanaona mambo ya digitali yanawachanganya.

Amesema wanapaswa kujifunza kuendana na mabadiliko hayo, kama wanataka kufanya kazi ya uandishi wa habari.

Amesema kwa sasa kila mmoja amekuwa mwandishi wa habari,  ambapo anatumia simu yake kurekodi na kutuma matukio katika mtandao, hivyo waandishi wa habari wanapaswa  kujikita zaidi kuandika habari ambazo zina ukweli na zilizokamilika.

“Waandishi wa habari mna mchango mkubwa, lakini lazima mkubali kuendana na mabadiliko, zamani ilikuwa unasubiri siku nyingi  kusubiri taarifa zichapishwe.

“Lakini kwa sasa kila mmoja anajifanya mwandishi, matukio ni papo kwa papo, mtu anarusha picha mtandaoni, bila kujali ina athari gani.

“Sasa ni kujitofautisha kati ya mwandishi mwenye taaluma na ambaye hana, badilikeni katika uandishi na mfanye vitu vya kuleta mabadiliko,” amesema Kamzora.

foto
Mwandishi: Diana Deus, Bukoba

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi