loader
Jaji Mkuu; Sensa itarahisisha shughuli za mahakama

Jaji Mkuu; Sensa itarahisisha shughuli za mahakama

JAJI Mkuu Prof. Ibrahimu Juma, amesema mhimili wa mahakama una jukumu la kuunga mkono sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu, kwa kuwa inatoa taswira ya kufahamu idadi ya watu na itasaidia kurahisisha shughuli za mahakama.

Amesema katika kujenga miundombinu ya mahakama, kunazingatia kipaumbele cha idadi ya watu na jiografia ya eneo husika, kwa kuwa kuna baadhi ya maeneo yanakuwa mbali na mahakama.

Prof. Juma amesema serikali ili iweze kutoa huduma kwa watu wake, inahitaji kujua idadi yao, ambapo kwa upande wa mahakama, sensa itasaidia kupanga upya uhitaji wa miundombinu.

 

 

“Mahakama ni huduma, hivyo ili uweze kutoa huduma kwa usahihi na kuwafikia watu ni muhimu kujua idadi yao, hivyo viongozi wa mahakama na watumishi wote wa mahakama tuone susala la sensa lina umuhimu kwetu.

“Kwa hiyo suala la mahakama kuingia katika mfumo wa anuani za makazi kutasaidia mahakama kuwafikia watu mpaka mahala wanapoishi,” amesema.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/46d520e4dca8850aa582427a4935ec4e.jpg

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa ...

foto
Mwandishi: Amina Omary, Tanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi