loader
Nyerere akumbukwa kwa  haki, umoja, kujitegemea

Nyerere akumbukwa kwa haki, umoja, kujitegemea

WANADIPLOMASIA na wadau wengine wamesema falsafa ya Baba wa Taifa, Julius Nyerere kuamini katika haki, amani na umoja vinaendelea kumpa heshima.

Walisema hayo Dar es Salaam katika kongamano la maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere lililoratibiwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF).

Mkurugenzi Mtendaji wa MNF, Joseph Butiku alisema Nyerere ataendelea kukumbukwa kama mtu mwenye kanuni na imani thabiti.

"Aliamini katika ubinadamu, haki za binadamu na haki za watu binafsi na jamii, aliamini katika amani na umoja,” alisema Butiku.

Balozi wa China nchini, Chen Mingjian alisema Nyerere alijenga urafiki wa kina na thabiti kati ya Tanzania na China na kujenga dhana ya kujitegemea kama njia mojawapo ya kuendelea.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Deng Li akizungumza kwa njia ya mtandao wa video, alisema Nyerere aliheshimika kwa ujasiri na ushupavu katika kuongoza na kupigania haki na maslahi ya watu na mataifa mengine.

“Tunapaswa kuendeleza moyo wa Nyerere wa urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika uliopendekezwa na Rais Xi Jinping wa China kwenye Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (Focac), kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika enzi mpya,” alisema Deng.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/6e8ad4948b132701e0837b71851f9b24.jpg

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Adam ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi