loader
Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaja UDSM

Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaja UDSM

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho ya saba ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), yatakayofanyika Mei 24 hadi 26 mwaka huu.

Makamu Mkuu wa  chuo hicho, Prof. William Anangisye amesema maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu ya utafiti na ubunifu kwa manufaa ya kijamii nchini Tanzania.

Amesema katika maadhimisho hayo, chuo kikuu kitaonesha miradi 100, kati ya miradi ya utafiti na ubunifu zaidi ya 300, ambayo ilifanya vyema zaidi .

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d3bbd7437e722edc9f7db199c51a20b2.jpeg

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa ...

foto
Mwandishi: Brighiter Masaki

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi