loader
Mashindano ya gofu wanawake yaiva

Mashindano ya gofu wanawake yaiva

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Dk. Stergomena Tax, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya gofu kwa wanawake yatakayofanyika viwanja vya gofu Lugalo mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza Dar es Salaam, Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo, Michael Luwongo, amesema wanawake wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

"Shindano la Lugalo Ladies Open 2022, lina lengo la kuenzi siku ya mama Duniani pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza utalii wa ndani na kukuza michezo nchini, "amesema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa yatafanyika Jumamosi na Jumapili.

Kwa upande wa nahodha wa wanawake wa klabu hiyo Hawa Wanyeche, amesema wachezaji mbalimbali wa ndani na nje watashiriki mashindano hayo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2426894ec27cff8d719c78237da271c3.jpg

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wachezaji ...

foto
Mwandishi: Brighiter Masaki

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi