loader
'Jamii ibadilike kuzuia maambukizi mapya'

'Jamii ibadilike kuzuia maambukizi mapya'

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, ametoa wito kwa jamii kutilia mkazo suala la kuzuia mlipuko wa maambukizo mapya ya virusi vya Ukimwi (HIV Epidemic Contol).

Amesema hatua hiyo itakasaidia kufikia malengo ya kidunia ya 95-95-95, ifikapo mwaka 2025.

Akifungua mkutano wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali ya VVU na Ukimwi leo Mei 19, 2022 mkoani Morogoro, Mkurugenzi huyo amesema:

"Lengo la kidunia litafikiwa endapo idadi ya maambukizo mapya, itakua chini ya idadi ya vifo vitokanavyo na Ukimwi."

Amesema nchi imekua ikifanya vizuri katika kuzuia maambukizo mapya kutoka 68,000 na vifo 32,000 mwaka 2020 hadi maambukizo mapya 54,000 na vifo 29,000 mwaka jana, lakini bado mlipuko  haujazuilika kwa kiwango kinachotakiwa.

Amesema baadhi ya njia za kuzuia maambukizi mapya ni  kubadili tabia, matumizi sahihi ya kondomu,  tohara kwa wanaume na uwezeshaji kiuchumi, hasa kwa wanaofanya biashara ya ngono, hasa mabinti, ili wawe  na njia mbadala ya kipato.

Akielimisha juu ya 95-95-95, Dk. Maboko amesema ni asilimia 95 za wote wanaoishi na VVU kupima na kujua hali zao kiafya, asilimia 95 ya wote waliopima na kugundulika kuwa wanaishi na VVU wawe wanatumia dawa za kupunguza makali ya virusi  (ARVs) na asilimia 95 ya wote wanaotumia dawa wawe wamepunguza virusi,  ifikapo 2025.

foto
Mwandishi: Abela Msikula, Morogoro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi