loader
Haji Manara, Barbara waitwa Kamati ya Maadili

Haji Manara, Barbara waitwa Kamati ya Maadili

OFISA Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez na Ofisa wa Yanga, Haji Manara wameitwa kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Mei 20,2022 kuwa kikao cha Kamati ya Maadili kitafanyika kesho, Dar es Salaam.

Amesema hatua ya kuwaita viongozi hao inatokana na Kamati ya Maadili kupokea malalamiko kutoka klabu ya Yanga, ikimtuhumu Gonzalez kwamba alikaririwa na redio moja ya Afrika Kusini akitoa shutuma dhidi ya Yanga, hivyo kuchafua taswira ya klabu hiyo.

Amesema nayo Simba inamlalamikia Manara kwenye Kamati ya Maadili kwa madai kuwa kupitia mtandao wake wa kijamii alitoa shutuma zisizo za kweli dhidi ya klabu yao, hivyo kukiuka kanuni za maadili za TFF.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cb19f5ab08569ac47499834d3676e3cb.jpg

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wachezaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi