loader
TFF walia Serengeti Girls kudhalilishwa

TFF walia Serengeti Girls kudhalilishwa

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewasilisha malalamiko Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kupinga vitendo vya udhalilishaji walivyofanyiwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ya wasichana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Girls.

Baadhi ya wachezaji wa Tanzania walilazimishwa kuonesha maungo yao uwanjani wakati mechi kati ya Tanzania na Cameroon wachezaji wakiingia kipindi cha pili, viongozi wa benchi la ufundi la Cameroon na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la soka la nchi hiyo (fecafoot), walikwenda uwanjani na kuwavuta wachezaji na kuwalazimisha kuonesha nyeti zao ili wathibitishe jinsia zao.

Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred, alisema tukio hilo limeonesha ubaguzi na udhalilishaji ambao hauwezi kufumbiwa macho.

Kidao alisema kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikifanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana michezoni lakini ilikuwa ikipuuzia ila umefika muda wa kuchukua hatua.

"Tumeshawasilisha malalamiko yetu na tunaamini hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya Cameroon," alisema Kidao.

Kamishna wa mchezo huo, Jacline Ndirumukando, alisema amewasilisha ripoti kuelezea tukio hilo.

"Niliwakatalia kwenda uwanjani, lakini walilazimisha, wameingilia kazi yangu, hivyo nimetoa taarifa," alisema.

Nahodha wa Serengeti Girls, Noela Patrick, alilaani tukio hilo huku akiwataka wachezaji waliodhalilishwa kutulia wakati TFF ikichukua hatua.

Noela alisema tukio hilo halitawapunguzia morali wa kushinda kwa kishindo mechi ya marudiano itakayofanyika nyumbani.

Hii si mara ya kwanza kwa timu za Tanzania kufanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana michezoni.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/fe84ee3dac49f0abe1239ff57fb23fed.jpg

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wachezaji ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo, Yaounde

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi