loader
Sare na Geita yamkera Pablo

Sare na Geita yamkera Pablo

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema hajaridhishwa kabisa na kiwango cha timu yao baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Geita Gold FC katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Franco alisema timu yake ilicheza chini ya kiwango.

“Sijaridhishwa kabisa na sare tuliyopata dhidi ya Geita. Lengo la kila mmoja wetu ilikuwa ni kupata pointi tatu. Timu yetu haipo imara kabisa, haswa tunapokuwa tunacheza katika viwanja vya ugenini,” alisema Franco.

Alisema timu yake haikucheza walivyotaka icheze. Franco alisema safu yake ya ulinzi haikuwa imara kabisa.

Alisema hata alama moja waliopata ni kama bahati tu kwao, huku akisisitiza kuwa morali ya wachezaji wake ipo chini sana atahakikisha wanarejesha morali ya timu yao.

“Kwa siku zilizobakia tukijipanga vyema na wachezaji wangu wakarudi katika hali zao na imani kubwa sana tutaifunga Yanga katika mchezo wetu wa nusu fainali dhidi yao,” alisema Franco.

Naye kocha msaidizi wa Geita, Mathias Wandiba alisema anaipongeza timu yake kwa kupata sare dhidi ya Simba SC.

“Mechi ilikuwa nzuri sana timu zote zilikuwa zikishambuliana muda wote, tatizo kubwa lilikuwa kwenye timu yetu, tulifanya kosa moja Simba wakasawazisha,” alisema Wandiba.

Alisema anawaomba mashabiki wao wajitokeze kwa wingi katika kuishangilia timu yao kwenye michezo mitano iliyobakia.

Katika msimamo wa Ligi Kuu, Geita Gold FC wapo katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 35, huku Simba SC ipo katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 51.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7e18908ffa07b9b77fbeafa0f13b7071.jpeg

RAIS Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wachezaji ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi